Jana Yanga ilitinga nusu fainali ya kombe la Muungano baada ya kuichapa Muembe Makumbi mabao 4-0 katika mchezo wa robo fainali uliopigwa uwanja wa New Amaan Complex.
Mshambuliaji Prince Dube aliendeleza kasi yake ya kuzifumania nyavu akiweka kambani mabao mawili.
Dube sasa amefunga mabao manne katika mechi mbili zilizopita ambazo zimeshuhudia Yanga ikiweka kambani mabao 10.
Ndani ya mechi tano, Yanga imefunga mabao 17 bila kuruhusu nyavu zake kutikiswa. Takwimu hizi ni katika mashindano yote.
Ni wazi kwa kasi hii ya Wananchi malalamiko yataongezeka kwani Yanga haionyeshi dalili ya kupunguza vipigo kwa wapinzani wake.
Baada ya ushindi dhidi ya Muembe Makumbi, mkufunzi wa Yanga Pedro Goncalves alionyesha kukwera na propaganda zinazofanywa dhidi ya kikosi chake lakini akasisitiza hawatapunguza kile wanachofanya.