Michuano ya SportPesa Super Cup itafikia tamati Jumapili ijayo, Juni 10 kwa mchezo wa fainali kati ya Simba ya Tanzania dhidi ya Gor Mahia ya kenya.
Gor Mahia imetinga fainali baada ya kuilaza Singida United mabao 2-0 kwenye mchezo wa nusu fainali uliopigwa leo kwenye dimba la Afraha.
Meddy Kagere, mshambuliaji hatari wa timu hiyo ambaye amekuwa akitajwa kuwaniwa na Yanga ndiye aliyeifunga mabao yote mawili.
Kagere anaongoza kwa mabao katika michuano hiyo akiwa amefunga mabao matatu.
Mapema kabla ya mchezo huo, Simba ilitinga fainali kwa kuiondosha Kakamega HomeBoyz kwa mikwaju ya penati 5-4 baada ya timu hizo kutoka suluhu katika muda wa dakika 90.
Licha ya kutinga fainali, Simba imecheza jumla ya dakika 180 bila ya kufunga bao kwenye michuano hiyo.
Mchezo wa fainali utapigwa Jumapili, Juni 10, 2018 katika uwanja wa Afraha.
Bingwa wa michuano hiyo atajinyakulia kitita cha Dola 30,000 pamoja na kupata tiketi ya kusafiri nchini Uingereza kwenda kuchuana na Everton katika dimba la Goodison Park.

ADVERTISE HERE