Yanga yatahadharisha wachambuzi wanaoichafua mitandaoni

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Apr 2026
Yanga yatahadharisha wachambuzi wanaoichafua mitandaoni

Klabu ya Yanga imepanga kuwachukulia hatua baadhi ya wachambuzi wanaozungumza au kuandika habari zenye lengo la kuwachafua mabingwa hao wa soka Tanzania Bara.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema uongozi umeanza kushughulikia suala hilo na watatoa taarifa kwa Wanachama juu ya hatua watakazochukua.

"Kuhusu wachambuzi wanaoandika au kuongea habari zenye lengo la kuichafua Klabu ya Yanga, viongozi wanashughulikia jambo hilo na muda sio mrefu nitawajuza hatua zitakazochukuliwa," alisema Kamwe.

Baada ya Yanga kutoka kwenye nyakati ngumu na kuanza kugawa vipigo kwa kila timu inayokuja mbele, kumeibuka baadhi ya wachambuzi ambao wanasambaza propaganda wakiaminisha jamii kuwa mabingwa hao wa soka nchini ushindi wao si halali kuwa 'wananunua mechi'.

Mijadala hiyo imeendelea kushika kasi mitandaoni hasa baada ya Yanga kuifumua Mbeya City mabao 6-0 katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa KMC Complex juzi.

Yanga imepanga kuwafikisha wachambuzi hao mbele ya mamlaka za soka ili wakathibitishe tuhuma zao.

Katika hatua nyingine, Kamwe amesema uongozi wa Yanga haujafanya mazungumzo na mchezaji Seleman Mwalimu wala klabu yake ya Wydad CA.

Kamwe amewataka Mawakala/Wachambuzi kutumia mbinu nyingine ya kuwatafutia mikataba wachezaji wao bila ya kuihusisha klabu ya Yanga.

Kumekuwa na taarifa nyingi kumuhusu Mwalimu hasa baada ya juzi kuonekana uwanja wa KMC Complex akishuhudia mchezo wa ligi kuu wakati Yanga ikichuana na Mbeya City.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
14h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’