Droo ya hatua za robo fainali na nusu fainali kombe la CRDB, imefanyika leo ambapo mabingwa watetezi wa michuano hiyo Yanga wamepangwa kucheza dhidi ya JKT Tanzania.
Mshindi wa mchezo huo utakutana na mshindi wa mchezo kati ya Mashujaa Fc dhidi ya Azam Fc kwenye hatua ya nusu fainali.
JKT Tanzania watakuwa wenyeji kwenye mchezo wa robo fainali dhidi ya Yanga huku Mashujaa Fc wakiwa wenyeji kwenye mchezo dhidi ya Azam Fc.
Hii hapa ratiba kamili ya mechi za robo fainali;

ADVERTISE HERE