Shoo za Mudathir, Okello zinarejea KMC Complex Alhamisi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Apr 2026
Shoo za Mudathir, Okello zinarejea KMC Complex Alhamisi

Baada ya kuingamiza Pamba Jiji kule Mwanza katika mchezo uliopita wa ligi kuu, nyota wa Yanga Mudathir Yahya na Allan Okello wanatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi kitakachoikabili Mbeya City hapo kesho katika mchezo wa ligi kuu ya NBC.

Mudathir amekuwa na msimu bora mpaka sasa akiongoza orodha ya vinara wa mabao kwenye kikosi cha Yanga akiweka kambani mabao 7.

Ushirikiano wake na Okello umeanza kuwa tishio kwa timu pinzani kwani wawili hao pamoja wamehusika kwenye mabao matatu katika mechi mbili zilizopita.

Mchezo dhidi ya Pamba Jiji Mudathir alifunga mabao mawili yote pasi zikitoka kwa Okello ambaye siku hiyo aliondoka na hat-trik ya asisti kwani pia alitoa pasi ya bao la tatu lililofungwa na Maxi Nzengeli.

Okello sasa amefikisha asisti 4 kwenye ligi huku pia akifunga mabao mawii.

Okello alianza taratibu majukumu yake ndani ya kikosi cha Yanga lakini sasa ni kama ameshazoea mazingira na anaonyesha uwezo wake halisi.

Yanga inahitaji ushindi dhidi ya Mbeya City ili iendelee kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi kabla ya mchezo dhidi ya watani zao Simba utakaopigwa May 03 dimba la Benjamin Mkapa.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’