Droo ya hatua ya robo fainali na nusu fainali kombe la CRDB itafanyika siku ya Ijumaa, April 17 kuanzia saa 6 mchana.
Droo hiyo itahusisha miamba nane iliyotinga robo fainali ya michuano hiyo.
Mabingwa watetezi Yanga ni miongoni mwa timu hizo Wananchi wakiweka rekodi ya aina yake baada ya kucheza miaka mitano bila kupoteza mchezo.
Azam Fc, Simba, Singida BS, JKT Tanzania, TRA United, Coastal Union na Mashujaa Fc pia zinasubiri droo hiyo.

ADVERTISE HERE