Dhamira yetu ni kushinda kila mechi ili kutetea ubingwa - Kamwe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Apr 2026
Dhamira yetu ni kushinda kila mechi ili kutetea ubingwa - Kamwe

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City utakaopigwa Alhamisi April 16 uwanja wa KMC Complex yanaendelea kwa tahadhari kubwa.

Kamwe amesema wanatambua mchezo dhidi ya Mbeya City hautakuwa mwepesi wakiwa na kumbukumbu ya matokeo ya mchezo wa duru ya kwanza uliopigwa uwanja wa Sokoine ambao ulimalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana.

"Hatukuondoka na pointi tatu kwenye mchezo wa kwanza sasa tunarudi KMC Complex tukiwa nyumbani, dhamira yetu ni kuona tunafanya vizuri zaidi."

"Sasa tuko raundi ya pili, ligi imeshachanganya, dhamira yetu sasa imebadilika, sio kumfunga Mbeya City tu, bali kuwa na mwendelezo mzuri ili kuhakikisha tunatetea ubingwa wetu kwa mara ya tano mfululizo"

"Ni dhamira hiyo ambayo itatufanya sisi Yanga tuende kwenye mchezo huo tukiwa na ari kubwa, tutacheza kwa kujituma na kujitolea ili kuhakikisha tunashinda na kuendelea kujiweka katika nafasi nzuri kwenye mbio za ubingwa," alisema Kamwe

Yanga ilirejea mazoezini jana kukamilisha maandalizi ya mchezo huo ambao ushindi kwa Wananchi utaendelea kuwaweka juu ya msimamo wa ligi kw tofauti kubwa ya alama.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’