Siku nne kuelekea Mkutano Mkuu Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Jun 2018
Siku nne kuelekea Mkutano Mkuu Yanga
Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Wanachama wa klabu ya Yanga yameshika kasi sasa zikisalia siku nne kuelekea Mkutano huo muhimu utakaotoa dira kwa klabu hiyo.

Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema wako katika hatua za mwisho kukamilisha maandalizi ya Mkutano huo utakaofanyika kwenye ukumbi wa Maafisa wa Polisi, jijini Dar es salaam.

Mkwasa amesema wanakusudia kuwaalika watu mbalimbali akiwemo aliyekuwa Mwenyekiti na mfadhili wa klabu hiyo, Yusuph Manji.

Pia mwaliko utapelekwa kwa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Mkutano huo maalumu kwa wanachama, umeitishwa ili kujadili masuala mbalimbali ya klabu hiyo, ikiwa pamoja na suala zima la mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji.

Baadhi ya ajenda zinazotarajiwa kuwasilishwa kwenye mkutano huo ni pamoja na kujadili ushiriki wa Yanga katika michuano ya kimataifa ikiwemo hatua waliyofika kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho, Mapato na Matumizi, bila ya kusahau Mabadiliko kuhusu mfumo wa uendeshaji.

Swala la uchaguzi wa kujaza nafasi zilizo wazi huenda likawasilishwa kupitia mengineyo ingawa kuna uwezekano mkubwa kwa ajenda hiyo kuondolewa ili kuwapa nafasi Wanachama kujadili masuala muhimu.

Juzi Kaimu Mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga alisema mkutano huo utakuwa na lengo la kuwaeleza wanachama matatizo yanayoikabili timu yao, kuhusu uchaguzi wa kuziba nafasi zililizo wazi utatangazwa baadaye.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’