Klabu ya Yanga imepiga hatua kubwa katika mchakato wa ujenzi wa uwanja wake wa kisasa, baada ya kukamilisha michoro pamoja na makadirio ya gharama za mradi huo.
Akizungumza na TBC Online, Rais wa klabu hiyo, Injinia Hersi Said, alisema maandalizi ya ujenzi yanaendelea vizuri na kwa umakini mkubwa ili kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwa viwango vinavyotakiwa.
βKwenye ujenzi wa uwanja tumefika kwenye eneo zuri sana. Tunafanya mchakato wetu kwa umakini mkubwa na kwa usahihi. Tuliwatangaza GSM kuwa washindi wa tenda ya ujenzi wa uwanja. Tayari tumepata mchoro wa awali wa uwanja. Klabu imeshatoa maoni kuhusu mchoro huo. Jana tumekamilisha michoro yote na gharama za ujenzi,β alisema Hersi.
Kampuni ya GSM imepewa jukumu la kusimamia ujenzi huo, huku hatua ya kukamilika kwa michoro ikiashiria kuwa utekelezaji wa mradi unaweza kuanza mara baada ya taratibu zilizobaki kukamilika.
Uwanja huo unaotarajiwa kujengwa karibu na Makao Makuu ya klabu hiyo, Jangwani jijini Dar es salaam, unatarajiwa kuwa uwanja wa kisasa na wenye kukidhi viwango vya kimataifa, hatua itakayoiwezesha Yanga kuwa na uwanja wake binafsi.