Kiungo mshambuliaji wa Yanga Mudathir Yahya leo ameendeleza kiwango bora cha kuzifumania nyavu akiweka kambani mabao mawili na kuisaidia Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Pamba Jiji.
Kwa mchezo wa pili mfululizo, Yanga leo ilianza mchezo huo bila ya mshambuliaji asili ikiwakosa Prince Dube na Laurindo Depu ambao wanaendelea kuimarika kabla ya kurejea uwanjani baada ya kupona majeraha.
Mabao mawili aliyofunga Muda leo yanamfanya afikishe mabao 7 sasa akiwa nyuma ya kinara wa mabao Fabrice Ngoy wa Namungo Fc mwenye mabao 8.

Muda ndio kinara wa mabao katika kikosi cha Yanga akifutiwa na washambuliaji Depu na Dube ambao kila mmoja amefunga mabao 6.
Pacome Zouzoua anashika nafasi ya 4 katika orodha hiyo akiwa amefunga mabao 5.
ADVERTISE HERE