Haya ni maoni yaliyokusanywa kutoka kwa wadau mbalimbali wa soka nchini wanaoamini iwapo yatafanyiwa kazi, Yanga itaweza kurejesha makali yake.
Kipa wa Uhakika
Mlinda lango namba moja wa Yanga, Youthe Rostand amekuwa na kiwango cha 'homa ya vipindi' leo anacheza vizuri kesho anaboronga.
Pengine majeruhi ya Kakolanya na kukosa uzoefu kwa Kabwili kuliifanya Yanga isiwe na mbadala wa mlinda lango huyo raia wa Cameroon.
Imetaarifiwa kuwa uongozi wa Yanga uko mbioni kusajili kipa mwingine ingawa haijulikani anachukua nafasi ya nani, Kakolanya ambaye mkataba wake umemalizika au Rostand ambaye itabidi avunjiwe mkataba wake wa mwaka mmoja uliobaki
Beki mzoefu
Licha ya kuwa na walinzi wa kati wanne, ni Yondani na Chikupe pekee walioweza kuituliza safu ya ulinzi ya Yanga.
Yanga inahitaji mlinzi mwingine wa kati mzoefu atakayeweza kuwasaidia Chikupe na Yondani wakati Abdallah Shaibu akiendelea kupata uzoefu.
Kukosekana kwa Yondani na Chikupe kwenye michuano ya SportPesa Super Cup kumechangia Yanga kuondoshwa mapema.
Kuna taarifa kuwa Yanga inamuwinda beki wa zamani wa Azam FC Sergie Wawa. Wawa ni mzoefu, akipatikana ataweza kusaidia Yanga hasa kwenye michuano ya Kimataifa.
Kiungo mchezeshaji
Thabani Kamusoko alitarajiwa kuibeba Yanga katika eneo hilo lakini majeruhi yamemrudisha sana nyuma. Yanga inahitaji kusajili kiungo mwingine mchezeshaji atayeweza kushirikiana na waliopo.
Washambuliaji
Obrey Chirwa ndiye aliyekuwa mshambuliaji tegemeo ingawa hakuwa na mwendelezo mzuri kutokana na changamoto za hapa na pale.
Hakuna uhakika kama Yanga itaweza kumbakisha mshambuliaji huyo lakini inahitaji kusajili washambuliaji angalau wawili hata kama Chirwa atabaki ili kuongeza ushindani baina yao.
Amissi Tambwe amekuwa majeruhi kwa muda mrefu na hakuna uhakika kama ataweza kurejesha makali yake kutokana na umri kumtupa mkono.
Ujio wa mshambuliaji Marcelin Koukpo hautoshi, yafaa asajiliwe mshambuliaji mwingine wa pili atayeongeza ushindani.
Safu ya ushambuliaji ya Yanga ikiwa na watupia mabao wakali wawili ukiongeza na Matheo Antony ambaye anaimarika siku hadi siku, kwa nini isifanye vizuri?

ADVERTISE HERE