Leo saa 10:15 jioni Yanga itashuka uwanja wa CCM Kirumba kumenyana na Pamba Jiji katika mchezo wa ligi kuu ya NBC.
Kocha Mkuu wa Yanga Pedro Goncalves leo amemuanzisha mlinda lango Hussein Masalanga huku Aboutwalib Mshery akikosekana baada ya kupata changamoto kuelekea mchezo huo
Mchezo dhidi ya Pamba Jiji utakuwa wa pili kwa mlinda lango namba moja Djigui Diarra kukosekana akitarajiwa kumaliza adhabu yake kwa kukosa mchezo wa kombe la CRDB dhidi ya TMA utakaopigwa April 11.
Huu utakuwa mchezo wa kwanza kwa Masalanga kuanza kwenye ligi angu alijiunge na mabingwa hao wa soka Tanzania Bara kwenye usajili wa dirisha dogo akitokea klabu ya Singida BS.
Katika mechi 17, Yanga haijaruhusu bao kwenye mechi 14, ambapo clean-sheet 10 ni za Diarra huku nne zikiwa za Mshery.
Mshery hajaruhusu bao katika mechi zote alizokaa langoni kwenye ligi msimu huu.