Kikosi cha Yanga jioni ya leo kimekamilisha maandalizi yake uwanja wa CCM Kirumba kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Pamba Jiji utakaopigwa kesho Jumatano.
Hari njema kwa Wananchi ni kurejea kikosini kwa mshambuliaji Prince Dube ambaye leo alishiriki kikamilifu maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo huo.
Baada ya kukosa mchezo uliopita dhidi ya Tanzania Prisons, Dube huenda akawa sehemu ya kikosi kitakachoikabili Pamba Jiji.




ADVERTISE HERE