Wakati Wananchi wakisubiri muda tu wakaishuhudie timu yao Yanga ikishuka uwanja wa KMC Complex kuikabili Tanzania Prisons katika mchezo wa ligi kuu ya NBC, rekodi za mechi zilizopita zinatoa taswira tofauti baina ya timu hizo.
Yanga imekuwa na rekodi ya kibabe kile inapokutana na Tanzania Prisons, katika mechi 35 zilizopita Yanga imepoteza mchezo mmoja tu. Mabingwa hao watetezi wameshinda michezo 24 huku wakitoka sare michezo 10.
Msimu uliopita Prisons walipoteza mechi zote mbili za ligi dhidi ya Yanga na msimu huu walipoteza mchezo wa duru ya kwanza kwa kufungwa bao 1-0 pale uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Leo timu hizo zinakutana tena huku kila moja ikihitaji alama zote tatu. Yanga haijashinda mechi tatu zilizopita za ligi ambao zote walitoka sare wakati Prisons nao hali yao sio nzuri, hatari ya kushuka daraja ni kubwa kama hawataanza kukusanya alama tatu katika kila mchezo.
Ni wazi leo Prisons watahitaji kuwa kwenye ubora mkubwa kuwazuia Yanga katika mchezo ambao kwa Wananchi ni kama fainali kwa kuzingatia matokeo ya mechi zilizopita.