Baada ya mapumziko ya takribani mwezi mzima, mikiki mikiki ya ligi kuu ya Wanawake (WPL) inarejea leo ambao Yanga Princess itakuwa uwanja wa Azam Complex kuikabili Ruangwa Queens. Mchezo huo unatarajiwa kupigwa kuanzia saa 12 jioni.
Yanga Princess ilikamilisha mechi za duru ya kwanza ikishika nafasi ya pili baada ya kukusanya alama 30 wakiwa alama moja tu nyuma ya watani zao Simba Queens wanaoongoza ligi wakiwa na alama 31.
Kinadada hao Wananchi walipoteza mchezo mmoja tu duru ya kwanza dhidi ya Simba Queens na sasa wana jukumu la kuhakikisha hawadondoshi tena alama kwenye duru ya pili ili kuwa na nafasi ya kutwaa ubingwa kwa mara ya kwanza.
Yanga Princess ya msimu huu ni bora zaidi pengine kuliko misimu yote iliyopita, matumaini ya kutwaa ubingwa ni makubwa