Ni siku ya kihistoria kwa soka la Afrika Mashariki baada ya DR Congo kufuzu rasmi kushiriki michuano ya FIFA World Cup 2026 wakiichapa Jamaica bao 1-0 kwenye mchezo wa play-off.
Mshambuliaji wa zamani wa Yanga Fiston Mayele ambaye kwa sasa anaitumikia klabu ya Pyramids Fc ya Misri, alikuwa sehemu ya kikosi cha DR Congo kilichokata tiketi kwa mara ya pili baada ya kusubiri kwa miaka 52.
Kwa ushindi huo, DR Congo imekamilisha orodha ya mataifa 10 kutoka Afrika yatakayoshiriki mashindano hayo, ambayo kwa mara ya kwanza yatahusisha jumla ya timu 48 kutoka duniani kote.
Ni jambo la kujivunia kwa Mayele ambaye pale atakapokuja kuandika historia yake, hataacha kuitaja klabu ya Yanga ambao ndio msingi wa mafanikio yake.
Mashabiki wa Yanga pia wanaweza kujivunia mshambuliaji huyo, na watafarijika zaidi kama watamuona kule Marekani akipeperusha bendera ya Taifa lake.
Safari yake kutoka ligi ya Tanzania, Misri hadi kufikia hatua ya kushiriki michuano mikubwa ya dunia ni hadithi ya mafanikio inayovutia na kuhamasisha vijana wengi wa Afrika.