Mlinda lango wa Yanga Djigui Diarra amewashukuru mashabiki wanaomchangia fedha ili aweze kulipa faini ya Tsh Mlioni 4 adhabu kutoka bodi ya ligi.
Mapema leo, Kamati ya uendeshaji na usimamizi wa ligi ya bodi ya ligi ilitangaza kumfungia Diarra mechi tatu na faini ya jumla ya Tsh Milioni 4 kutokana na makosa yaliyojitokeza kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar.
"Asanteni Wananchi. Nawapenda sana," aliandika Diarra kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii
Hadi kufikia Ijumaa jioni, takribani Tsh Milioni 1.5 tayari ilikuwa imekusanywa lengo likiwa kukusanya Tsh Milioni 4 kulipa faini hiyo.

ADVERTISE HERE