Kamwe aonya, ligi ikirejea ni mwendo wa vichapo tu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
27 Mar 2026
Kamwe aonya, ligi ikirejea ni mwendo wa vichapo tu

Yanga imesema maboresho yaliyofanywa ndani ya kikosi hicho yametokana na mapendekezo ya kocha mkuu Pedro Goncalves, yakilenga kuongeza ushindani katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Akizungumza kuhusu mabadiliko hayo, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ali Kamwe, alisema hatua hiyo imechukuliwa kwa kuzingatia tathmini ya kitaalamu kulingana na uzoefu wa benchi la ufundi.

“Ongezeko ambalo limefanywa ni pendekezo la kocha Pedro mwenyewe. Ameliomba hilo kutokana na uzoefu alionao kwenye ligi, aina ya wapinzani ambao tunakutana nao pamoja na mazingira ya viwanja,” alisema Kamwe.

Aliongeza kuwa maboresho hayo yanatarajiwa kuwa na mchango mkubwa katika kuisukuma timu hiyo kufikia malengo yake ya kutwaa ubingwa msimu huu.

“Ni ongezeko ambalo limefanywa kitaalamu. Litakuwa na mchango mkubwa katika kuisukuma timu katika kupambania taji la ligi,” alisisitiza.

Kamwe pia ameweka wazi kuwa Yanga inalenga kurejea katika kiwango bora mara baada ya mapumziko mafupi ya ratiba ya FIFA, huku ikijiandaa na muendelezo wa ligi unaotarajiwa kuanza mwezi Aprili.

“Ligi ni mwezi wa nne, hivyo ukiangalia ni kama siku chache ligi itaanza tena. Tunaamini baada ya mapumziko haya tutarejea uwanjani tukiwa imara zaidi,” alieleza.

Msemaji huyo wa mabingwa wa nchi amebainisha kuwa mchezo ujao dhidi ya Tanzania Prisons utakuwa fursa kwa timu hiyo kuonyesha matokeo ya maboresho yaliyofanywa.

“Kwenye maboresho ambayo yamefanywa baada ya break, Yanga SC itarudi kutoa kichapo. Mechi inayofuata ni Tanzania Prisons, tunataka kutumia mchezo huo kuwaonyesha mashabiki kwamba tumefanya maamuzi sahihi kuipeleka timu katika kiwango cha juu,” alisema.

Yanga inaendelea kushika nafasi ya juu katika msimamo wa ligi, huku ikilenga kuendeleza ubora wake katika mechi zilizobaki ili kutimiza malengo ya msimu.

Xtra 90 job opportunities

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
3h ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
8h ago
READ MORE →
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE →
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE →
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →