Yanga Soccer School yapata wadhamini zaidi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Mar 2026
Yanga Soccer School yapata wadhamini zaidi

Klabu ya Yanga imetangaza kampuni ya EMWANI kuwa mbia mpya wa mradi wa kusaidia na kuibua vipaji vya soka kupitia mradi wa Shule ya Vipaji ya Yanga SC.

Akizungumza kwenye mkutano na wanahabari mapema leo, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe alisema EMWANI imejitolea kutoa udhamini kwa wanafunzi 10 ambao watajiunga na Yanga Soccer School.

Klabu kwa kushirikiana na kampumi hiyo wameandaa mashindano maalum yatakayofanyika siku ya Jumamosi ambapo kupitia mashindano hayo, watapatikana vijana 10 ambao watajiunga na Yanga Soccer School kupitia udhamini waa EMWANI.

“Mradi wetu wa Yanga Soccer school imekuwa kwa kiasi kikubwa kama ambavyo Pitso Mosimane alitutabiria. Mchakato huu umepata baraka nyingi kutoka kwa wadau mbalimbali katika kuusaidia mradi huu wenye lengo la kusaidia kijana mwenye kipaji”

“Hatimaye leo kijana mwenzetu wa Kitanzania Leo Mendez ambaye ni mmiliki wa Kampuni ya EMWANI wamejitolea kuunga mkono mradi wa Yanga Soccers School. Kwa mantiki hiyo kampuni ya EMWANI ni mbia mwenzetu wa mradi wa kusaidia na kuibua vipaji vya soka kupitia mradi wa Shule ya Vipaji ya Yanga SC

"Yanga SC na Kampuni ya EMWANI wameandaa mashindano yatakayofanyika 28/03/2026 (Jumamosi) pale kituo cha TFF Kigamboni. Klabu ya Yanga inatangaza rasmi vituo mbalimbali ambavyo vina akademi wanakaribishwa. Usahili umeanza pale Jangwani. EMWANI watachagua wachezaji kumi ambayo watawadhamini kujiunga na Yanga Soccer School”

“Mshindi wa mashindano ya Yanga SC na EMWANI atapata kiasi cha Tsh Milioni 3, mshindi wa pili atapewa milion 1, watakaoishia nusu fainali watapata 500,000. Zawadi hizi ni udhamini wa EMWANI hivyo wadau mbalimbali ambao wanamiliki vituo vya akademi wanahimizwa kufanya usajili mapema jangwani au kupitia email ya Yanga. Washiriki wanapaswa kuwa chini ya miaka 18,” alisema Kamwe

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
8h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
16h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
19h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
23h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’