Kocha Msaidizi wa Yanga Abduhalim Moalin anatarajiwa kutua nchini wiki hii kuanza majukumu yake akishirikiana na wataalam wengine kwenye benchi la ufundi chini ya kocha Pedro Goncalves.
Yanga imemrejesha Moalin aliyewahi kuhudumu kwenye nafasi ya Mkurugenzi wa ufundi na kocha msaidizi ukiwa ni mpango wa kuimarisha benchi la ufundi baada ya tathmini iiyofanyika kubaini mapunufu.
Moalin anatua kumuongezea nguvu Goncalves ambaye uongozi umeendelea kuwa na imani nae.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema timu inatarajiwa kurejea mazoezini wiki hii kuanza maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons ambao utapigwa April 04 uwanja wa KMC Complex.
Baada ya kumaliza mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar, nyota wa Yanga ambao hawana majukumu ya timu za Taifa, walipewa mapumziko ya siku chache na sasa wako tayari kurejea kwenye majukumu yao wakiwa na ari mpya.