Licha ya kuruhusu bao dakika za jioni kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar, mlinda lango wa Yanga Djigui Diarra bado ni kinara wa clean sheet.
Diarra amekusanya clean sheet 10 huku akifuatiwa na walinda lango Aishi Manula (Azam Fc) na Erick Johora (Mashujaa Fc) ambao wana clean sheet 6 kila mmoja.
Baada ya dakika 90 za mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar, Diarra alikerwa na tukio la mwamuzi kuruhusu bao la kona dakika za lala salama katika mazingira ambayo mlinda lango huyo kutoka Mali alionekana kusukumwa wakati akijaribu kuokoa.
Meneja wa Yanga Walter Harrison alilazimika kufanya kazi ya ziada kumtuliza Diarra ambaye hakuwa na 'simile' dhidi ya mwamuzi.
Unapozungumzia mafanikio ya Yanga katika misimu hii minne, hutakosa kutaja jina la Diarra.
Diarra ni mwanafamilia halisi wa Yanga na yuko tayari kuipambania nembo ya Yanga pale anapoona haitendewi haki