Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Clement Sanga ambaye ndiye anayekaimu Uenyekiti, amesema ni vyema uchaguzi wa Mwenyekiti ukafanyika sambamba na Makamu wake ili kuwapata watu 'watakaoendana' kufanya kazi pamoja.
Sanga amekuwa akikaimu nafasi ya Mwenyekiti tangu mwezi May 2017 baada ya kujiuzulu aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuph Manji.
Sanga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), amesema majukumu katika bodi hiyo yamemfanya ashindwe kutimiza ipasavyo majukumu yake katika klabu ya Yanga.
Yanga inatarajiwa kufanya uchaguzi kujaza nafasi zilizo wazi katika Mkutano wake Mkuu wa mwaka utakaofanyika Jumapili ijayo, Juni 10 2018 kwenye ukumbi wa Polisi jijini Dar es salaam.
Hivi karibuni Serikali kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT), iliiagiza TFF kuvitaka vilabu vyote vya soka kufanya uchaguzi kujaza nafasi zilizo wazi kwa muda mrefu.
Agizo hilo linaifanya Yanga ishindwe kukwepa kufanyika kwa uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti na sasa huenda pia ikalazimika kujaza nafasi ya Makamu Mwenyekiti.

ADVERTISE HERE