Mkufunzi wa Yanga Pedro Goncalves amesema ili kuboresha kiwango cha soka nchini ni muhimu kuboresha viwanja pia.
Kocha huyo Mreno amesema katika mechi wanazocheza ugenini, viwanja vingi haziko katika ubora unaotakiwa na hivyo kuwapa wakati mgumu wachezaji kutafsiri kwa usahihi kile wanachoelekezwa na walimu wao.
"Jambo lingine muhimu ni ubora wa viwanja. Kuna tofauti kubwa unapocheza kwenye uwanja wenye ubora mzuri na ule usio na hali nzuri. Katika baadhi ya michezo ikiwemo wa mwisho, timu zote zilipata ugumu kutokana na hali ya uwanja jambo lililoathiri umakini na umaliziaji."
"Katika michezo yetu ya hivi karibuni mingi imekuwa ya ugenini mara nyingi katika mazingira magumu. Mfano mzuri wa kiwango chetu ugenini ulikuwa mchezo wa Singida, ambapo tulicheza kwenye uwanja mzuri uliotuwezesha kucheza soka bora zaidi."
"Ikiwa tunataka kuinua kiwango cha soka ni muhimu pia kuboresha viwanja. Hata hivyo, tunapaswa kuendana na hali na kutafuta njia za kuwazidi wapinzani wetu. Pamoja na changamoto zote, tunaendelea kuwa na mtazamo chanya."
"Tuko kileleni mwa ligi na tunaamini bado tuna nafasi kubwa ya kuboresha kiwango chetu. Kesho, lengo letu ni kutengeneza nafasi nyingi zaidi, kuwa makini katika umaliziaji na kupigania pointi tatu," alisema Goncalves