Baada ya mchezo dhidi ya Azam Fc uliopigwa jana na kumalizika kwa suluhu ya bila kufungana, hakuna muda wa kupumzika kwa Yanga inapaswa kusafiri leo kuelekea mkoani Arusha tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya TRA United.
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa keshokutwa Jumatano, March 18 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Ikumbukwe kwenye uwanja huo juzi mchezo kati ya TRA United dhidi ya Simba haukufanyika baada ya mvua kubwa kunyesha iliyopelekea kuharibu miundombinu ya uwanja.
Hata hivyo mpaka sasa hakuna mabadiliko ya ratiba kwa maana mchezo kati ya TRA United dhidi ya Yanga itafanyika kama ulivyopangwa.
Baada ya mtanange huo Yanga inapaswa kuelekea mkoani Dodoma kwani Jumamosi, March 21 wanakabiliwa na mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar uwanja wa Jamhuri.