Huu moto wa Depu hakuna wa kuzima

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Mar 2026
Huu moto wa Depu hakuna wa kuzima

Mshambuliaji wa Yanga Laurindo Aurelio 'Depu' jana aliendeleza 'moto' wake wa kuzifumania nyavu akifunga bao pekee la ushindi wa Yanga katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons.

Katika mchezo huo uliopigwa uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma, Wananchi waliibuka na ushindi wa bao 1-0 na kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi kwa tofauti ya alama 7 baada ya kufikisha alama 35.

Depu ambaye aliondoka na tuzo ya nyota wa mchezo, alifunga bao hilo kwenye dakika ya 78 akimalizia mpira uliotemwa na mlinda lango wa Prisons Mussa Mbissa.

Hilo lilikuwa bao la sita kwa Depu kwenye ligi akimfikia mshambuliaji mwenzake Prince Dube. Ikumbukwe Depu amejiunga na Yanga mwishoni mwa mwezi Januri katika usajili wa dirisha dogo na amekuwa na wastani wa kufunga katika kila mechi.

Jumla sasa amefunga mabao 11 katika mechi 10 alizocheza kwenye mashindano yote.

Ni wazi huu unaweza kuwa msimu wa maajabu kwa Depu, anahitaji kufunga mabao mawili tu kumfikia Fabrice Ngoy wa Namungo Fc ambaye ndiye anaongoza orodha ya vinara wa mabao kwenye ligi kuu ya NBC.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’