Wakati Wananchi wakitakiwa kusafiri kuelekea mkoani Tabora kuikabili Tnzania Prisons katika mchezo wa ligi kuu uliopangwa kupigwa Alhamisi March 12, mchezo utakaofuata dhidi ya Azam Fc umerejeshwa uwanja wa Benjamin Mkapa.
Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano Azam Fc Thabit Zacharia 'Zakazakazi' amethibitisha mchezo huo uliopangwa kupigwa March 15 kurejeshwa uwanja wa Benjamin Mkapa.
Awali Serikali ilitangaza kufunga uwanja huo kupisha ukarabati mkubwa, hata hivyo bado zoezi hilo halijaanza.
Kabla ya kuikabili Azam Fc, mabingwa hao watetezi wanakabiliwa na mechi dhidi ya Tanzania Prisons keshokutwa, wakitakiwa kuelekea mkoani Tabora na watakapomalizana na Prisons wanapaswa kurejea Dar kuikabili Azam Fc.
ADVERTISE HERE