Saa chache zijazo Yanga itakuwa uwanjani pale Singida kuwakabili wenyeji wao Singida Black Stars katika mwendelezo wa ligi kuu ya NBC.
Katika mchezo huo nyota wawili wa Yanga Mohamed Damaro Camara na Frank Assink wanaweza kuwakabili waajiri wao hao wakiwa wanaitumikia Yanga kwa mkopo.
Lakini pia winga Offen Chikola ambaye anaitumikia Singida BS kwa mkopo, anaweza kuwakabili waajiri wake Yanga akitua timu hiyo kwenye usajili wa dirisha dogo.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe ametoa ufafanuzi kuwa makubaliano ya kimkataba kati ya Yanga na Sngida BS katika usajili wa nyota hao, yanaruhusu kutumika dhidi ya waajiri wao.
Kuhusu idadi ya kadi za njano, Kamwe amesema Damaro hajafikisha kadi nne za njano ambazo zitamlazimu kukosa mchezo mmoja.
Hivyo kama kocha Pedro Goncalves atahitaji kumtumia kwenye mchezo huo, ruksa kutumika.