Kaimu Kocha wa Yanga Noel Mwandila ametaja sababu ya timu hiyo kupoteza mchezo wa robo fainali michuano ya SportPesa Super Cup kwa kulazwa mabao 3-1 na Kakamega HomeBoyz.
Mwandila amesema makosa mawili 'ya kitoto' yaliyofanywa na safu ya ulinzi ya Yanga ndiyo yaliyopelekea timu hiyo kupoteza mchezo leo.
"Tulifanya makosa mawili ya kitoto yaliyopelekea tufungwe mabao mawili. Mabao hayo yaliwaongezea kujiamini Kakamega HomeBoyz.
"Tulijitahidi kusawazisha wakati tulipokuwa nyuma kwa mabao 2-1. Lakini unaweza kuona, idadi kubwa ya wachezaji wetu wamecheza chini ya kiwango kwa kuwa wametoka kwenye majeruhi huku wengine wakitoka kuugua Malaria.
"Kwa ujumla hatujawa na msimu mzuri, kutokana na changamoto mbalimbali.
"Lakini leo tofauti ilikuwa makosa mawili ya kitoto tuliyofanya kwenye safu ya ulinzi. lakini hatukucheza vibaya sana.
"Tumekubali matokeo, tutajipanga kwa ajili ya michuano ijayo."

ADVERTISE HERE