GSM aweka udhamini Yanga Soccer School

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Mar 2026
GSM aweka udhamini Yanga Soccer School

Wazazi wametakiwa kupeleka watoto wao wenye vipaji vya soka kwenye usaili ili kujiunga na program ya Yanga Soccer School chini ya udhamini wa GSM.

Program hiyo ambayo ilizinduliwa na Yanga miezi michache iliyopita awali Wazazi walitakiwa kulipa ada lakini ujio wa udhamini wa GSM maana yake ni kuwa wale watakaopita kwenye usaili watajiunga na program hiyo pasipo gharama za ziada.

Akizungumza katika mkutano wa wanahabari mapema leo, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe alisema siku ya uzinduzi wa vipaji itafanyika tarehe 8 Machi 2026.

Wazazi wametakiwa kusajili watoto wao Makao Makuu ya klabu ya Yanga, Jangwani jijini Dar es salaam.

"Mradi huu ambao GSM wameweka fedha zao, nawahakikishia utkuwa mradi wenye mafanikio makubwa na kihistoria hapa Tanzania."

"Tutachukua vijana wengi wenye vipaji kwa ajili ya kuhakikisha tunaisaidia klabu ya Yanga na mpira wa Tanzania kwa ujumla."

"Vijana hawa tutawalinda kwa wivu mkubwa kuhakikisha wanafikia malengo ya kuanzishwa kwa program hii."

"Kwa hiyo niwaombe wazazi wafike Makao Makuu ya Yanga wakiwa na watoto wao waliokidhi vigezo."

"Vigezo ni cheti cha kuzaliwa mtoto, barua ya utambulisho kutoka Serikali za mita na barua ya uthibitisho y Mzazi kumruhusu mwanaye kushiriki program hii," alisema Kamwe

GSM Foundation watalipia vijana 20 ada/Chakula/ Uniform na uangalizi mwingine ili waweze kujiunga na Yanga Soccker School, umri unaotakiwa kwenye program hii ni kijana kuanzia Miaka 15 hadi 17.

Usajili umeanza leo 3.3.2026 mpaka tarehe 6.3.2026 saa 3:00 asubuhi mpaka saa 12:00 Jioni

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
59m ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
6h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
9h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’