Wakati mashabiki wa soka nchini wakisubiri mtanange wa dabi ya Kariakoo kati ya Yanga dhidi ya Simba ambao utapigwa baadae leo katika uwanja wa New Amaan Complex visiwani Zanzibar, Yanga inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na takwimu za kibabe msimu huu.
Ukiwa ni mchezo wa 11, Yanga itakuwa ikisaka ushindi wa 10 kwani mpaka sasa Wananchi wameshinda mechi 9 katika ya 10 walizocheza, wakitoka sare moja tu.
Idadi ya mabao ya kufunga ni 27 huku wakiwa wameruhusu mabao mawili tu. Upande wa Simba, wameshinda mechi 7 kati ya 10, wamepoteza mechi 1 na kutoka sare mechi 2.
Simba wamefunga mabao 18 huku wakiruhusu mabao manne kutikisa nyavu zao pia.
Washambuliaji Laurindo Aurelio na Prince Dube ndio vinara wa mabao kwenye kikosi cha Yanga kila mmoja akifunga mabao matano wakati Salum Mwalimu ni kinara upande wa Simba akiwa amefung mabao manne.
Takwimu za michezo ya dabi kati ya Yanga na Simba tangu mwaka 2017 pia zinaibeba Yanga ikiwa imefunga jumla ya mabao 17 na kuruhusu mabao 11 huku watani zao wakifunga 11 n kuruhusu 17.
Katika kipindi hicho Yanga imeshinda mechi 6 huku Simba ikishinda mechi 3 na mechi 7 zikiwa ni sare.
Nje ya takwimu hizo, bado heshimaa ya mchezo wa dabi iko palepale, Wananchi wanatambua mchezo wa leo ni mpya na watahitaji kupambana ili kupata matokeo mazuri pasipo kujali walichovuna mechi zilizopita.