Msimu huu tumeharibu, tujipange upya

Muungwana wa Yanga By Muungwana wa Yanga
β€’
4 Jun 2018
Msimu huu tumeharibu, tujipange upya
Kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa timu 'ndogo' ya Kakamega HomeBoyz kwenye michuano a SportPesa Super Cup kimeongeza machungu kwa mashabiki wa Yanga.

Lakini sidhani kama matokeo haya inafaa yawe ya kushangaza kwa aina ya Yanga iliyomaliza msimu kwa kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Azam FC.

Katika michezo 11 iliyopita, Yanga imeshinda mchezo mmoja pekee. Kufungwa leo haikuwa ajabu hata kidogo.

Kabla ya kushinda 1-0 dhidi ya Mbao FC Yanga ilikuwa imecheza michezo tisa bila ushindi. Kipigo dhidi ya Azam FC na KK HomeBoyz kimeongeza idadi ya michezo 12, ushindi mmoja!

Kwa mtizamo wangu nadhani hata viongozi wa Yanga hawakuwa wametilia mkazo mkubwa mashindano haya kwa kuwa walifahamu hakutakuwa na muujiza.

Ndio maana hawakuona umuhimu wa kuwajumuisha baadhi ya wachezaji waandamizi ambao walibaki jijini Dar es salaam. Pengine kulikuwa na sababu za msingi kufikia uamuzi huo.

Hata kocha Mkuu Mwinyi Zahera hakuwa ameongozana na timu. Ni Yanga pekee ambayo haikuwa na kocha wake Mkuu kwenye michuano hiyo.

WanaYanga wana maswali mengi sana yanayohitaji majibu juu ya mwenendo wa timu yao msimu huu. Wanaweza kuyapata majibu Jumapili ijayo, Juni 10 kwenye Mkutano Mkuu.

Juni 10 wanachama watakuwa na nafasi ya kuwahoji viongozi wao Yanga imekumbwa na nini?

Wanachama wakiutumia vizuri Mkutano huo, watakuwa wamechangia ujenzi wa Yanga imara ya msimu ujao.

Msimu huu tukubali, tumeharibu, TUJIPANGE.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’