Daktari Yanga afunguka changamoto za majeruhi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
25 Feb 2026
Daktari Yanga afunguka changamoto za majeruhi

Mshambuliaji Prince Dube alipata jeraha kwenye kifundo cha mguu katika mchezo wa kombe la CRDB dhidi ya Cosmopolitan. Daktari wa Yanga Moses Etutu amesema jeraha hilo ni dogo halihitaji matibabu zaidi ya mapumziko ambapo mchezaji huyo alipewa mapumziko ya siku 10.

Wakati Dube akipewa mapumziko, Etutu amethibitisha kuwa kiungo mshambuliaji Pacome Zouzoua ambaye pia alipewa mapumziko ya wiki moja baada ya kuumia bega kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya JS Kabylie, yuko tayari kurejea kikosini.

Hata hivyo Etetu amesema Yanga itaendelea kuwakosa Clement Mzize, Edmund John na Aziz Andabwile ambao nao walipata changamoto za majeraha.

“Dube alipata shida kidogo ya kifundo cha mguu, ni jeraha dogo tu ambalo limetufanya tumpe mapumziko ya siku 10 ama mechi mbili ili aweze kurejea haraka uwanjani."

“Jeraha lake sio kubwa sana, halihitaji matibabu zaidi ni mapumziko ya muda ili kurudi kwenye utimamu ndiyo maana hakuonekana kwenye safari ya kuifuata Namungo,” Etutu alinukuliwa na Mwanaspoti.

Kuhusu Pacome, Etetu amesema aliumia bega la kushoto akiwa katika harakati za kuwania mpira sambamba na kipa wa JS Kabylie, jeraha lake linachukua muda wa wiki moja kupona tangu siku amepata shida.

“Nafikiri huo muda sasa umeshatimia, ni suala la mwalimu kumtumia au kuendelea kumpa mapumziko ili hadi siku anarejea uwanjani anakuwa amepona kwa asilimia 100, hivyo tutegemee kumuona uwanjani hivi karibuni"

Akizungumzia kuhusu Mzize, alisema mshambuliaji huyo alirudi uwanjani baada ya matibabu ya goti kwenda vizuri lakini akiwa katika harakati za kujiandaa na mchezo wa mwisho wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya JS Kabylie aliumia tena, hivyo wamemfanyia vipimo na kumuandalia program maalum ya mazoezi.

“Mzize baada ya upasuaji wa goti ambao ulienda vizuri alirejea uwanjani na kuendelea na majukumu akipata dakika chache za kucheza mechi ya ugenini dhidi ya AS FAR Rabat na baada ya hapo akiwa kwenye maandalizi ya mechi ya pili alipata shida kidogo, tatizo tayari limefanyiwa vipimo na anatarajia kuanza program ya mazoezi hivi karibuni,” alisema daktari huyo.

Wakati huohuo, alizungumzia shida ya Edmund, alisema alipata tatizo la bega la kushoto kwenye maandalizi ya mchezo wa JS Kabylie na lilitoka sehemu yake, akibainisha kwa kawaida kuumia kwa namna hiyo kunachukua wiki tatu ili kupona.

“Wiki hizo tatu zinamsaidia mchezaji kupona kabla ya kurudi kwenye migongano na kudondoka kama mchezaji kutokana na matukio hayo kuweza kumsababishia shida ya maumivu kwa ndani, kwa sasa anafanya mazoezi yake binafsi,” alisema.

Kwa upande wa Andabwile, alisema aliumia kidole gumba wakati anajaribu kupiga mpira, wamemfanyia vipimo na kujiridhisha ni maumivu madogo ambayo yatamchukua siku tano ili kurudi kwenye hali yake ya kawaida.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
8h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE →
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
17h ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE →
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
21h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
23h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE →