Pacha ya walinzi wa kati Abdallah Shaibu na Said Juma Makapu ni wazi imekuwa haina faida kwa Yanga mpaka sasa.
Wawili hao wamekuwa wakifanya makosa yanayoigharimu Yanga kwenye michezo waliyocheza pamoja.
Shaibu anahitaji kucheza na beki mzoefu wa kumuongoza kwa kuwa bado hana uzoefu wa kutosha wakati Makapu kwake yeye nafasi anayocheza sio asili yake, analazimika kucheza kutokana na upungufu uliopo.
Mabao mawili kati ya matatu yaliyofungwa leo kimsingi yamesababishwa na uzembe katika ulinzi, kukosekana kwa Dante na Yondani pengo limeonekana dhahiri.
Bila shaka mchezo huu utawasaidia mabosi wa Yanga wanaosimamia masuala ya usajili kuweza kufanya maamuzi sahihi juu ya aina ya wachezaji wanaowasajili.
Lakini pia kukosekana kwa Kocha Mkuu Mwinyi Zahera bado kunaendelea kuiathiri Yanga.
Kocha huyo ambaye inaelezwa tayari amewasili jijini Dar es salaam alitarajiwa angeungana na Yanga huko Kenya pengine kama ingeshinda mchezo wa leo dhidi ya Kakamega HomeBoyz.

ADVERTISE HERE