FT : KK HomeBoyz 3-1 Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Jun 2018
FT : KK HomeBoyz 3-1 Yanga
Yanga imekuwa timu ya kwanza kuyaaga mashindano ya SportPesa Super Cup baada ya kulazwa mabao 3-1 katika mchezo uliopigwa kenye dimba la Afraha, Nakuru Kenya.

Uzembe wa safu ya ulinzi ya Yanga uliizawadia Kakamega HomeBoyz mabao mawili yote yakifungwa na Allan Wanga, mshambuliaji mkongwe wa kakamega HomeBoyz aliyewahi kuitumikia Azam FC.



Bao la kwanza alifunga baada ya walinzi wa Yanga kutegeana kumkaba wakati la pili akilifunga kwa mkwaju wa penati baada ya kuvutwa na Haji Mwinyi ndani ya eneo la hatari hivyo mwamuzi kutoa adhabu ya mkwaju wa penati.

Matheo Antony aliifungia Yanga bao pekee kupitia mkwaju wa adhabu dakika chache kabla ya mapumziko.

Licha ya kucheza vizuri kwenye kipindi cha pili Yanga ilikosa mbinu ya kuipenya ngome ya Kakamega.

Wakati ikisaka bao la kusawazisha ilijikuta ikiruhusu bao la tatu kwenye dakika za majeruhi baada ya KK HomeBoyz kufanya shambulizi la kushitukiza na Opondo kuutumbukiza mpira wavuni.

Kipa Youthe Rostand alilazimika kufanya kazi ya ziada kuokoa mpira wa kichwa 'mkizi' cha Opondo uliokuwa unaelekea kimiani wakati mchezo huo ukielekea ukingoni.

Akizungumza baada ya mchezo huo Kaimu Kocha wa Yanga Noel Mwandila amesema idadi kubwa ya wachezaji wake wametoka majeruhi huku akikiri kamba mapungufu yaliyojitokeza kwenye safu ya ulinzi yamechangia Yanga kupoteza mchezo huo.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
12h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
16h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
17h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
17h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’