Tumejiandaa kuikabili Namungo Fc - Goncalves

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Feb 2026
Tumejiandaa kuikabili Namungo Fc - Goncalves

Kocha Mkuu wa Yanga Pedro Goncalves amesema kikosi chake kimejiandaa kikamilifu kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc ambao utapigwa kesho Jumapili katika uwanja wa Majaliwa.

Akizungumza katika mkutano na wanahabari kuelekea mchezo huo, Goncalves amesema licha ya kukabiliwa na ratiba ngumu ya kucheza mechi mfululizo, wanakwenda kwenye mchezo huo wakiwa imara lengo likiwa kuchukua alama tatu.

Goncalves amewashukuru mashabiki wa timu hiyo waliojitokeza kwa wingi kuwapokea akiamini wameongeza hamasa kwa wachezaji wao.

"Kwanza kabisa napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa watu wote waliotupokea tangu tulipowasili. Mapokezi tuliyopata tangu tulipotua hadi kufika hapa yalikuwa mazuri sana na yametugusa kila mmoja wetu. Ninaamini kila mtu ana hamasa kubwa kuelekea mchezo wa kesho na nguvu hiyo tuliyopewa inatupa motisha kubwa"

"Kesho tutacheza dhidi ya Namungo FC, timu ambayo hadi sasa imekuwa na msimu mzuri sana. Nafikiri wako nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi. Ni timu imara sana wanapocheza nyumbani. Mara nyingi wamekuwa wakishinda mechi zao za nyumbani, jambo linaloonyesha ubora wao"

"Tunafahamu vizuri changamoto inayotusubiri kesho. Tunapitia ratiba yenye msongamano mkubwa wa mechi, lakini tunapaswa kucheza mechi moja baada ya nyingine. Kesho tutakuwa ugenini dhidi ya Namungo, lakini tutacheza kwa falsafa ileile tunayofuata katika kila mchezo. Mwisho wa siku tutafanya kila tuwezalo kupata alama tatu na kuendelea vizuri na safari yetu," alisema Goncalves

Aidha Goncalves amesema baadhi ya wachezaji watakosekana kutokana na changamoto za majeraha

"Kwa bahati mbaya tuna baadhi ya wachezaji wenye majeraha ambao hawakuweza kuja na timu. Aziz (Andambwile) alipata majeraha kidogo, bado tunaendelea kufuatilia hali yake lakini tuna matumaini si tatizo kubwa"

"Edmond pia ana majeraha aliyopata wiki iliyopita huenda akarejea mazoezini baada ya siku chache. Pacome alipata maumivu baada ya kugongana na kipa katika mchezo uliopita, hivyo hayuko katika hali nzuri kwa sasa."

"Kibwana na Mshery pia ni wagonjwa na hakuweza kusafiri. Dube alikuwa na tatizo la kiafya wakati wa mazoezi. Mzize anaendelea vizuri huku akipata uangalizi wa umakini kabla hajarejea tena kuwa nasi. Hata hivyo, wachezaji waliopo watafanya kila wawezalo kusaidia timu kupata alama tatu kesho," alisema

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
8h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
16h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
19h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
22h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’