Pacome apewa mapumziko

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Feb 2026
Pacome apewa mapumziko

Daktari wa Yanga Moses Etutu amesema mshambuliaji Pacome Zouzoua anaendelea vizuri baada ya changamoto aliyoipata kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya JS Kabylie uliopigwa visiwani Zanzibar na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-0.

Etutu amesema nyota huyo raia wa Ivory Coast alipata changamoto ya bega baada ya kugongana na mlinda lango wa JS Kabylie.

Kwa sasa amepewa mapumziko ya siku chache kabla ya kurejea uwanjani kuendelea na majukumu yake.

"Pacome alipata shida baada ya kugongana na mlinda lango wa JS Kabylie lakini kwa sasa anaendelea vizuri."

"Amepewa muda tu wa kupumzika ili ajiweke sawa kabla kurejea tena uwanjani kuendelea na majukumu yake," alisema Etutu.

Leo Yanga itashuka uwanja wa KMC Complex kuikabili Cosmopolitan katika mchezo wa hatua ya 64 bora kombe la CRDB.

Ni wazi Pacome hatakuwa sehemu ya kikosi kitakachoshuka dimbani lakini anaweza kuwa tayari kurejea pale Yanga itakaposafiri Lindi kuikabili Namungo Fc Februari 22 na hata mchezo dhidi ya JKT Tanzania Februari 25.

Bila shaka Pacome atakuwa imara pale Yanga itakapoikaribisha Simba kwenye mchezo namba 54 NBC PL utakaopigwa March 1, New Amaan Complex Zanzibar

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
22h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’