Msimu wa maajabu kwa Abuya

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Feb 2026
Msimu wa maajabu kwa Abuya

Kiungo kiraka wa Yanga Duke Abuya ameendelea kung'ara katika kikosi cha Wananchi msimu huu akiwa mchezaji anayehusika katika matukio mengi awapo uwanjani.

Juzi katika mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya JS Kabylie, Abuya alitumika kama kiungo mkabaji lakini alionekana kila mahali uwanjani, timu ilipojilinda na hata kushambulia.

Ni yeye aliyeanzisha shambulizi lililopelekea kupatikana kwa goli la tatu akimtengenezea pasi mpenyezo Prince Dube ambaye alimtengea Chadrack Boka kufunga bao la tatu na kuihakikishia Yanga ushindi wa mabao 3-0.

Katika mechi zote za ligi ya mabingwa, Abuya alikuwa mhimili wa eneo la kiungo la Yanga. Hata katika ligi kuu ya NBC, Abuya bado ameendelea kuwa mtu muhimu katika kikosi cha kocha Pedro Goncalves. Ndiye kinara wa kutoa pasi za mabao kwenye ligi akiwa na asisti nne mpaka sasa.

Ikumbukwe ametumika kwenye mechi nyingi kama kiungo mkabaji lakini bado amekuwa na mchango mkubwa kwenye eneo la mwisho la timu pinzani.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
9h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
14h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’