Matchday; Yanga vs JS Kabylie, CAFCL R6

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Feb 2026
Matchday; Yanga vs JS Kabylie, CAFCL R6

Yanga SC leo Jumapili, Februari 15, 2026, inashuka dimbani katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, kuikabili JS Kabylie ya Algeria kwenye mchezo wa mwisho wa Kundi B wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) huku ikihitaji ushindi mnono ili kufuzu robo fainali.

Mchezo huo ni wa maamuzi kwa wawakilishi hao wa Tanzania ambao wanaingia wakiwa nafasi ya tatu na alama 5. Vinara wa kundi hilo ni Al Ahly wenye alama 9, wakifuatiwa na AS FAR wenye alama 8, huku JS Kabylie wakishika mkia kwa alama 3.

Yanga inapaswa kushinda kwa tofauti ya angalau mabao mawili ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kusonga mbele. Hata hivyo, ushindi huo utahitaji kuambatana na matokeo ya mchezo wa Cairo, ambako Al Ahly wataikaribisha AS FAR.

Iwapo Al Ahly wataibuka na ushindi dhidi ya AS FAR na Yanga ikatimiza wajibu wake kwa ushindi mabao 2-0 au zaidi, timu hiyo ya Tanzania itafuzu kwa kuwa itakuwa imefunga mabao mengi zaidi. Hadi sasa, Yanga imefunga mabao mawili na kuruhusu matatu, wakati AS FAR wamefunga matatu na kuruhusu mawili.

Rekodi ya michezo ya ana kwa ana kati ya Yanga na AS FAR inaonyesha uwiano, kila timu ikishinda 1-0 nyumbani kwake, jambo linaloifanya tofauti na idadi ya mabao ya kufunga kuwa na uzito mkubwa katika kuamua nafasi ya pili ya kundi.

Ni aina ya mechi ambayo kocha Pedro Goncalves anapaswa 'kujilipua' kwa kuhakikisha timu yake inakwenda kushambulia kuanzia dakika ya kwanza ili kufanikisha mpango wa kufunga mabao mengi.

Hii sio mara ya kwanza kwa Yanga kucheza mechi za aina hii na ikafanikiwa kushinda ingawa pia zipo nyakati haikuweza kutimiza malengo yake.

Yanga inapaswa kufunga hesabu zake ndani ya dakika 90 kwani nafasi ya kufuzu ni kubwa matarajio yakiwa Al Ahly kuibuka na ushindi dhidi ya AS FAR huko Misri.

Kila la kheri Wananchi...!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
2h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
17h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
21h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’