Yanga, GSM wajadili mikakati ya ujenzi wa uwanja

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Feb 2026
Yanga, GSM wajadili mikakati ya ujenzi wa uwanja

Uongozi wa Yanga leo unatarajiwa kukutana na kampuni ya GSM visiwani Zanzibar katika kikao cha kimkakati cha kujadili na kuweka sawa hatua za utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa uwanja wa klabu hiyo katika Makao Makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam.

Kikao hicho kitaongozwa na Rais wa Yanga, Injinia Hersi Ally Said, na kuhudhuriwa na Mwenyekiti wa makampuni ya GSM, Ghalib Said Mohamed, pamoja na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji na wataalamu wa mradi huo.

Hatua hiyo inafuatia uamuzi wa Kamati ya Utendaji ya Yanga iliyokutana hivi karibuni iliyopita kupitia maombi ya wazabuni mbalimbali waliowania zabuni ya ujenzi wa uwanja huo, ambapo kampuni ya GSM Tanzania Limited ilitangazwa rasmi mshindi baada ya kukidhi vigezo vilivyowekwa.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Makao Makuu ya Yanga, Jangwani, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ali Kamwe, alisema mchakato wa kumpata mkandarasi ulifuata taratibu zote za kitaalamu na kisheria.

Alieleza kuwa kabla ya kutangazwa kwa mshindi, klabu ilifanya tathmini ya kina ya eneo la ujenzi na kubaini kuwa kulikuwa na haja ya kupata eneo la ziada ili kuhakikisha uwanja huo unakidhi matakwa ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF). Kupitia ushirikiano na Serikali, Yanga ilipatiwa eneo la nyongeza pamoja na hati miliki, jambo lililoweka mazingira mazuri ya kuanza utekelezaji wa mradi huo.

Kamwe alitumia pia nafasi hiyo kuishukuru Serikali ya Tanzania chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia klabu hiyo eneo la ziada, akisema hatua hiyo imekuwa chachu ya kuharakisha ndoto ya Yanga kuwa na uwanja wake binafsi.

Katika kikao cha leo Zanzibar, pande zote mbili zinatarajiwa kujadili ratiba ya kuanza kwa ujenzi, usanifu wa mwisho wa mradi, muundo wa usimamizi pamoja na makadirio ya muda wa kukamilika kwa uwanja huo.

Mradi wa uwanja wa Yanga unatajwa kuwa sehemu ya mkakati mpana wa kuimarisha miundombinu ya klabu na kuongeza vyanzo vya mapato kupitia mechi za nyumbani na shughuli nyingine za kibiashara.

Utekelezaji wa mradi huo ukienda kama ulivyopangwa, Yanga itajiunga na klabu chache nchini zenye viwanja vyao binafsi vinavyokidhi viwango vya kimataifa, hatua inayotarajiwa kuipa klabu hiyo nguvu zaidi kiuchumi na kimichezo.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’