Goncalves aahidi kuongeza makali safu ya ushambuliaji

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Feb 2026
Goncalves aahidi kuongeza makali safu ya ushambuliaji

Kocha Mkuu wa Yanga Pedro Goncalves amesema wanafanya maandalizi kabambe ili kuhakikisha wanafunga mabao mengi kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya JS Kabylie ambao utapigwa Jumapili Februari 15 katika uwanja wa New Amaan Complex.

Yanga inahitaji kushinda mchezo huo kwa kufunga mabao mawili au zaidi ili kuwa na nafasi ya kufuzu robo fainali kutegemeana na matokeo ya mchezo kati ya Al Ahly dhidi ya AS FAR.

Akizungumza visiwani Zanzibar ambapo kikosi chake leo kimeingia siku ya pili ya maandalizi tangu walipotua jana, Goncalves amesema walikuwa na nafasi ya kujihakikishia tiketi hiyo mapema lakini sare ya mechi moja nyumbani na vipigo viwili ugenini vimewalazimu wao kupigania nafasi hiyo katika mechi ya mwisho.

Amesema wamekuwa na mashindano mazuri mpaka sasa, changamoto pekee ambayo pengine imewafanya wasiwe wamefuzu ni kutotumia vyema nafasi nyingi wanazotengeneza.

Amesema kazi kubwa inafanyika kwenye uwanja wa mazoezi ili kuhakikisha siku ya Jumapili wanasahihisha eneo hilo la umaliziaji.

“Wakati tunaanza mechi za makundi, kila mmoja alikuwa haoni nafasi yetu ya kwenda robo fainali na hili lilitokana na kuangukia kundi ambalo lina timu zenye rekodi kubwa Afrika na zilizofanya uwekezaji mkubwa."

“Ukiangalia sasa ni tofauti kidogo ni vile tumefanya makosa ya kuangusha pointi hizi tano kwa kutoa sare nyumbani na kupoteza ugenini, tulikuwa na nafasi kubwa kuondoa huu wasiwasi lakini bado tuna nafasi ya kufanya vizuri hapa nyumbani katika mechi hiyo ya mwisho.”

“Tutakwenda tena kushambulia kwa nguvu ili tupate mabao, tunafanya kazi kubwa ya kuwapa mazoezi tofauti wachezaji wetu ili waweze kuongeza utulivu wanapofika eneo la mwisho, tunahitaji mabao lakini pia tunatakiwa kuwa makini tusiruhusu hayo yote yanawezekana,” alisema Concalves

Yanga inaendelea na maandalizi visiwani Zanzibar huku wapinzani wao JS Kabylie wakitarajiwa kutua visiwani humo usiku wa leo.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’