Mdhamini/Mfadhili wa Yanga GSM atakuwepo visiwani Zanzibar siku ya Jumapili wakati Yanga itakapomenyana na JS Kabylie katika mchezo wa kuhitimisha hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika.
Yanga inahitaji kushinda mchezo huo wa raundi ya sita kundi B ili kuwa na nafasi ya kufuzu robo fainali kutegemea na mchezo kati ya Al Ahly dhidi ya AS FAR.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amedokeza kuwa GSM atakuwa na Wananchi bega kwa bega katika mchezo huo ambao Yanga inahitaji matokeo ya aina moja tu,USHINDI.
"Wananchi na Tajiri yetu GSM Tutakuwa New Amaan Complex Jumapili TUKIFUZU KWA KISHINDO kuelekea Robo Fainali ya Caf Champions League," aliandika Kamwe kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii.
Inaelezwa GSM ameweka mezani dau la maana kwa wachezaji kama watafanikiwa kutinga robo fainali taarifa za ndaaani zikidokeza kuwa takribani Tsh Milioni 500 zinawasubiri wachezaji kama watafanikiwa kufuzu robo fainali.