Mkongwe Yanga afurahia ujio wa Ngassa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
2 Jun 2018
Mkongwe Yanga afurahia ujio wa Ngassa
Wakati baadhi ya mashabiki wa soka wakiishangaa Yanga kuamua kumrejesha kikosini nyota wake wa zamani, Mrisho Ngassa, kutoka Ndanda FC, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wana Jangwani, Lawrance Mwalusako, amebariki ujio wa winga huyo mwenye mbio.

Mwalusako aliyeichezea Yanga kwa mafanikio miaka ya 1980, alisema bado kiwango cha Ngassa kipo juu na ndio maana mabosi wa klabu hiyo wamemrejesha kwa vile vijana waliopewa nafasi wameshindwa kufanya la maana.

“Sioni tatizo kwa Ngassa kurejeshwa kikosini, tangu alipoondoka na nafasi yake kuchukuliwa na Simon Msuva, hakuna mchezaji mwingine aliyemudu kuvaa viatu vyake, hivyo kwangu ni sahihi kurudi nyumbani,” alisema Mwalusako.

“Unaposajiliwa Yanga au Simba, lazima mchezaji ujitambue na kujitathimini kuwa nyuma yako unafuatiliwa na mamia ya watu, lakini baadhi ya wachezaji waliopo sasa ni kama hawajui thamani ya jezi za timu hizo, Ngassa atawafundisha.”

Mwalusako pia amemtaka Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa, kutumia taaluma yake kuwaweka sawa vijana klabuni hapo.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
14h ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
19h ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
23h ago
READ MORE →
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE →
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE →
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE →
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE →