Hati ya kusafiria yamkwamisha Buba Jammeh kutua Morocco

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Feb 2026
Hati ya kusafiria yamkwamisha Buba Jammeh kutua Morocco

Kocha Mkuu wa Yanga Pedro Goncalves alitamani nyota mpya Buba Jammeh raia wa Gambia aliyesajiliwa muda mchache kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa, ajiunge na timu nchini Morocco.

Hata hivyo mpango huo umekwama baada ya mchezaji huyo kukumbana na changamoto ya hati yake ya kusafiria nchini Gambia na hivyo kushindwa kusafiri Morocco.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe ametoa ufafanuzi kwa nini nyota huyo hakutua Morocco kama ilivyotaarifiwa awali ambapo pengine angekuwa sehemu ya kikosi kitakachoikabili AS FAR katika mchezo muhimu wa raundi ya tano CAFCL.

"Buba kwa mpango wa kwanza ilikuwa aje moja kwa moja hapa Morocco na kila kitu kilikuwa tayari kiko sawa na alitarajiwa kuwasili leo (jana) ili ashiriki mazoezi na timu."

"Wakati tunamsajili alikuwa Angola na alikuwa akishughulikia hati yake ya kusafiria hivyo ikabidi atoke Angola aende Gambia kukamilisha zoezi hilo."

"Mpaka jana alikuwa amekamilisha zoezi hilo kwa sehemu kubwa zilikuwa zimesalia document chache tu za kukamilisha. Tukaangalia utaratibu wake kusafiri mpaka hapa Morocco, tukabaini angetua siku ya Jumamosi asubuhi."

"Kocha alimuhitaji atue mapema ili aweze kufanya mazoezi na timu ili kujiridhisha kama anaweza kumtumia katika mchezo dhidi ya AS DAR lakini imeshindikana kutokana na changamoto ya hivyo vibali vyake."

"Hivyo uongozi umeamua Buba atasafiri moja kwa moja jijini Dar es salaam ambapo ataungana na timu baada ya mchezo wetu dhidi ya AS FAR," alisema Kamwe

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
25m ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
5h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
9h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’