Kamati maalum ujenzi wa uwanja wa Yanga yaundwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Feb 2026
Kamati maalum ujenzi wa uwanja wa Yanga yaundwa

Klabu ya Young Africans SC (Yanga) imeunda kamati maalum itakayokuwa na jukumu la kusimamia na kuratibu ujenzi wa uwanja wake wa Kaunda, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa klabu hiyo wa kuimarisha miundombinu na kujitegemea kiuchumi.

Kamati hiyo itaongozwa na Mwenyekiti Eng. Hersi, huku wajumbe wake wakiwa ni wajumbe wote wa Kamati ya Utendaji ya Yanga SC pamoja na Alex Mgongolwa na Ivan Tarimo. Kamati hiyo imepewa dhamana ya kushughulikia masuala yote muhimu yanayohusu mradi huo mkubwa wa kimkakati kwa klabu.

Moja ya majukumu ya awali ya kamati hiyo ni kukutana na kampuni ya GSM Tanzania Limited kwa ajili ya kujadili mfumo wa ushirikiano katika ujenzi wa uwanja huo. Katika kikao hicho, pande hizo mbili zinatarajiwa kujadiliana kuhusu taratibu za kisheria na kibiashara zitakazotumika katika utekelezaji wa mradi huo.

Masuala yatakayojadiliwa ni pamoja na muda ambao uwanja utakuwa chini ya usimamizi au umiliki wa GSM Tanzania Limited, faida zitakazopatikana kwa Yanga SC pamoja na namna GSM itakavyonufaika na makubaliano ya ujenzi wa uwanja huo.

Uongozi wa Yanga SC umeeleza kuwa ujenzi wa uwanja huo ni mradi wa muda mrefu unaolenga kuimarisha mapato ya klabu, kuboresha mazingira ya michezo na kutoa huduma bora kwa mashabiki wake. Uwanja wa Kaunda unatarajiwa kuwa miongoni mwa miradi mikubwa ya maendeleo kuwahi kufanywa na klabu hiyo.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
14h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
20h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’