Lwandamina kuongezwa mkataba Yanga

Yanga Damu By Yanga Damu
β€’
1 Aug 2017
Lwandamina kuongezwa mkataba Yanga
Kocha Mkuu wa Yanga George Lwandamina 'Chicken' yuko kwenye mazungumzo na uongozi wa Yanga ili kusaini mkataba mpya.

Mkataba wake unakaribia kumalizika na Yanga inakusudia kumsainisha mkataba wa muda mrefu baada ya kuridhishwa na uwezo wake.

Alijiunga na Yanga msimu uliopita katika mzunguuko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom akichukua mikoba ya Hans van Pluijm ambaye alipandishwa cheo na kuwa Mkurugenzi wa Ufundi.

Alitokea klabu ya ZESCO ya Zambia, aliyoiongoza kutwaa ubingwa wa Zambia kwa miaka miwili mfululizo pamoja na kuifikisha nusu fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika.

Lwandamina licha ya kuiwezesha Yanga kutwaa ubingwa wa tatu mfululizo, msimu wake wa kwanza haukuwa mzuri sana kutokana na matatizo yaliyoikumba klabu.

Majeruhi, migomo ya wachezaji sababu ya ukata vilipelekea Yanga ishindwe kufurukuta katika michuano ya Kimataifa, michuano ambayo Lwandamina aliletwa mahsusi kwayo.

Msimu huu umeanza vizuri baada ya kukamilisha vyema zoezi la usajili, mwenyewe akilisimamia zoezi hilo.

Kipimo sahihi cha uwezo wake sasa kinaweza kuonekana msimu huu ambao anaanza na timu tangu mwanzoni.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
2h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
5h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
10h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
11h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’