Wakati Laurindo Aurelio 'Depu' na Prince Dube 'wakikiwasha' kwenye safu ya ushambuliaji ya Yanga, habari mbaya zaidi kwa timu pinzani ni kuwa mshambuliaji Clement Mzize ameanza mazoezi.
Baada ya kuwa nje kwa zaidi ya wiki nane, Mzize ameanza rasmi mazoezi ikiwa ishara ya urejeo wake kikosini.
Mzize anaweza kuwa tayari kuikabili AS FAR kwenye mchezo wa raundi ya tano ligi ya mabingwa baada ya mchezo wa kesho dhidi ya Al Ahly ambao ataukosa.
Wakati utatu wa Pacome, Dube na Depu 'PDD' ukianza kuwaogopesha timu pinzani, habari mbaya kwao ni kuwa Mzize nae anakuja kuongeza makali kwenye utatu huo.

ADVERTISE HERE