Wapinzani wa Yanga klabu ya Al Ahly inatarajiwa kuwasili visiwani Zanzibar leo kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa baina ya timu hizo ambao utapigwa Jumamosi, Januari 31 katika uwanja wa New Amaan Complex.
Wakati Al Ahly wakiwasili leo, Yanga iko visiwani Zanzibar tangu jana Jumatano ikiendelea na maandalizi kuelekea mchezo wa raundi ya nne kundi B ambao matokeo yake yanaweza kuamua hatma ya kufuzu robo fainali.
Ushindi kwa Yanga utawafanya wafikishe alama 7 na kuwa kwenye nafasi nzuri ya kufuzu robo fainali wakati kama Al Ahly watashinda huenda wakakata tiketi ya robo fainali mapema.









ADVERTISE HERE