Kikosi cha Yanga tayari kimewasili visiwani Zanzibar kukamilisha maandalizi ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Ahly utakaopigwa Jumamosi, Januari 31 katika uwanja wa New Amaan Complex.
Yanga iliondoka jijini Dar es salaam mapema leo siku moja baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Dodoma Jiji katika mchezo wa ligi kuu ya NBC.
Wananchi wametua Zanzibar wakiwa na dhamira moja tu, kushinda mchezo dhidi ya Al Ahly ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga robo fainali CAFCL.
Wapinzani wao Al Ahly wanatarajiwa kutua Zanzibar siku ya kesho Alhamisi









ADVERTISE HERE