Baada ya kupoteza mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Ahly Misri, kikosi cha Yanga kinarejea nchini kujiandaa na mchezo wa marudiano dhidi ya mabingwa hao wa kihistoria barani Afrika utakaopigwa Januari 31 dimba la New Amaan Complex visiwani Zanzibar.
Kabla ya mchezo huo siku ya Jumanne, Januari 27 Yanga itashuka dimba la KMC Complex kucheza mechi ya kiporo ligi kuu ya NBC dhidi ya Dodoma Jiji.
Baada ya mtanange huo Wananchi wataelekea Zanzibar kukamilisha maandalizi ya kuikabili Al Ahly kwa mara ya pili katika kipindi cha wiki moja.
Hii ni mechi ambayo Wananchi watazihitaji alama zote tatu ili kuweka hai matumaini ya kutinga robo fainali CAFCL.
Upande wa ligi kuu Yanga imepania kuendeleza mwanzo wake mzuri katika mkakati wa kutetea taji hilo kwa msimu wa tano mfululizo.
