Yanga kuifuata Al Ahly Januari 21

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Jan 2026
Yanga kuifuata Al Ahly Januari 21

Baada ya kutwaa kombe la Mapinduzi kikosi cha Yanga kimerejea mazoezini kujiandaa na mechi zinazofuata katika ligi kuu ya NBC na ligi ya mabingwa barani Afrika (CAFCL).

Kulingana na ratiba, Wananchi wanakabiliwa na mechi ya ligi kuu dhidi ya Mashujaa Fc siku ya Jumatatu, Januari 19 mchezo utakaopigwa uwanja wa KMC Complex.

Baada ya mtanange huo Yanga itakuwa na siku moja ya kujifua kabla ya kukwea pipa siku ya Jumatano Januari 21 kuelekea Misri tayari kwa mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Ahly.

Mechi hiyo ya raundi ya tatu kundi B, itapigwa Ijumaa Januari 23 jijini Cairo. 

Baada ya kuishia hatua ya makundi msimu uliopita, msimu huu Yanga imepania kuvuka hatua hiyo na kutinga robo fainali.

Mechi mbili zinazofuata dhidi ya Al Ahly zinaweza kuihakikishia Yanga nafasi nzuri ya kupata tiketi hiyo.

Al Ahly inaongoza kundi B ikiwa na alama nne sawa na Yanga lakini ikiwa na faida ya mabao mengi ya kufunga.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’